Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Malaysia, Mhe. Mej. Gen. Mbaraka Naziad Mkeremy amewasilisha rasmi Hati za Utambulisho kwa Mtukufu Sultan IBRAHIM, Mfalme wa Malaysia katika halfa iliyofanyika leo Oktoba 19 2026 katika Kasri la Mfalme la Istana Negara lililopo jijini Kuala Lumpur.  Hatua hiyo inamwezesha Mhe. Balozi Mkeremy kuanza rasmi kutekeleza majukumu yake ya kuiwakilisha Tanzania nchini humo.