Balozi Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Malaysia, Mhe. Mej. Gen. Mbaraka Naziad Mkeremy amewasili rasmi nchini humo Oktoba 15, 2026.
Mara baada ya kuwasili, Mhe. Balozi Mkeremy alipokelewa na Mabalozi wa Kundi la Afrika nchini humo katika hafla iliyoongozwa na Naibu Kiongozi wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao Malaysia ambaye pia ni Balozi wa Ufalme wa Eswatini nchini humo, Mhe. Menzie S. Dlammini.
Mapokezi hayo yaliwahusisha pia Maafisa kutoka Serikali ya Malaysia na Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Malaysia.
Mapokezi hayo ni sehemu ya utaratibu wa kidiplomasia unaolenga kumkaribisha Balozi Mteule na kuimarisha mahusiano ya kikazi na ushirikiano baina ya Tanzania na nchi nyingine za Afrika zinazowakilishwa nchini Malaysia.



