Jumuiya ya Watanzania nchini Malaysia yazinduliwa rasmi kupitia Mkutano ukiofanyika Ubalozini tarehe 14 Oktoba 2017 katika kilele cha maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya kifo cha baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Katika Mkutano huo, Mheshimiwa Dkt. Ramadhani Kitwana Dau, Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, pia alihudhuria na kutoa nasaha kwa watanzania.