Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Malaysia, Mhe. Mej. Gen. Dr. Mbaraka Naziad Mkeremy  amefanya ziara  katika kampuni ya Petronas yenye makao makuu yake kwenye minara pacha ya Malaysia (KLCC Twin towers). Petronas ndio kampuni yenye dhamana uchimbaji wa mafuta na gesi na elimu ya teknolojia ya mafuta na gesi kupitia chuo kikuu chao University Technology Petronas.
Balozi alipata taarifa za uendeshaji wa taasisi pamoja na namna inavyoshughulikia suala  zima la utafiti, uchimbaji na uzalishaji wa mafuta na gesi ndani ya Malaysia na nje ya Malaysia . Pamoja na hayo mazungumzo yameanzia kuanzisha mazungumzo endelevu ya kujenga uwezo kwa Watanzania kwenye elimu ya teknologia ya mafuta na gesi na uratibu wake kwa ujumla.