Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Malaysia, Mhe. Mej. Gen. Dr. Mbaraka Naziad Mkeremy amefanya ziara ya mwanzo Katika Chuo Kikuu cha Kuala Lumpur (Univeristy Kuala Lumpur nchini Malaysia). Lengo kuu ya ziara hiyo ni kuanziasha ushirikiano wa elimu katika fani mbali mbali akitilia mkazo zaidi kwenye fani ya ufundi wa vyombo vya usafiri wa angani Aircraft engineering na vyombo vya usafiri bahari Marine Engineering technology.


