Iftar Gathering with the Tanzania Embassy in Malaysia & the NAMA Foundation.

Ubalozi wa Tanzania uliopo Kuala Lumpur Malaysia iliwakutanisha wanafunzi wa Tanzania wanaosoma nchini kwenye futari y apamoja ambayo iliandaliwa kwa ushirikiano  na Nama Foundation

   https://namafoundation.org   tarehe 18/3/2025.  Balozi Mahadhi Juma Maalim alichukua fursa hii kuwahutumia wanafunzi kusimia lengo kuu lililowaleta hapa ambalo ni Elimu , pamoja na kutii sheria za nchi na kutojihusidha na mambo ambayo kwa namna moja au nyengine yataharibu malengo yao. Balozi Mahadhi alijumiuka pamoja na Mkurugenzi wa taasisi hiyo Dr. Saled Mubarak  na Mr. Azhar Mohamed ambae ni afisa kutoka Wizara ya Elimu ya Juu Malaysia katika kitengo cha EMGS kinachoshughulikia visa za elimu nchini Malaysia. wote kwa  pamoja walitoa nasaha kwa wanafunzi wa Tanzania jinsi ya kujiepusha na matatizo ambayo yatasababisha kuharibu taswira ya Tanzania kimaadili. 

Iftar NAMA x Tanzania Embassy 2025 Photos