Balozi Mahadh  J. Maalim alifanya mazungumzo na wakala wa Serikali ya Malaysia yenye jukumu la kujenga miundombinu ya usafiri wa reli , barabara sambasamba na majengo ya kufanya biashara kwenye vituo vya reli na mabasi na miundombinu ya mifumo ya kidigitali . Taasisi hii inayojulikana kama  The East Coast Rail Link (ECRL). 

Kikao hicho kiliongozwa na Mtendaji Mkuu (Chief Executive Officer ) wa Taasisi hiyo Dato  Baidzawi Che Mat ambae pia ni Mwenyekiti wa Asia Center of Excellence for Smart  Technologies (ACES).  na Menega Mkuu wa Idara ya  Ushirikiano na Mipango ya Kimkakati Bi. Salida Azizi . na watendaji wengine. Mazungumzo hayo yalifanyika tarehe 30 April 2025 katika Makao makuu ya ofisi hiyo iliopo  Putra Jaya.


  Katika mazungumzo hayo Balozi Mahadh aliomba mashirikiano ya kujenga uwezo baina ya nchi mbili     Tanzania na Malasia kupitia kwenye taasisi zenye jukumu kama  hilo. Pia kuangalia uwezekano wa mashirikiano ya moja kwa moja katika kuhakikisha Tanzania inapiga hatua zaidi ya maendeleo ya  miundombinu ya usafiri , makazi na sehemu za biashara. Ecrl imefanikisha kwa ufanisi mkubwa sana miradi ya kimkakati ya miundombinu ya reli na Barabara kwenye eneo la mashariki , kutokea Kuala lumpur hadi Gombak.